BigMoody

Monday, July 16, 2012

DRAKE>>KILA MWAKA NA DEM WAKE

KRIS HUMPHRIES
Baada ya kutokea uvumi kuwa anatoka na BasketBaller wa New Jersey Nets,Kris Humphries,Model Dollicia Bryan amefunguka kuwa yeye ndio queen mpya wa Drizzy Artist toka Young Money na si Kris kama inavyodaiwa
DRAKE vs DOLLICIA BRYAN
Kris Humphries alikua mume wa Model/Actress/TV personality Kimberly 'Kim' Kardashian aliyekua na beef na Dollicia na Mwakilishi wa Dollicia Bryan alifunguka kuwa kwa sasa shosti huyo anatoka na Drake na kwa sasa wako pande za Los Angeles wakila bata kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka na kabla ya kutoka na Drake,Dollicia Bryan alikua 'anatoka' na actor Hill Harpe

P UNIT

PRO-HABO UNIT AKA P-UNIT
Kundi la P-Unit toka Kenya walitarajiwa kupata shavu la kutangaza laptop za HP kwenye kampeni iliyobatizwa jina la 'Get your beat On' ambazo mteja akinunua anapata na headphones kali za Beats by Dre
P-Unit wameungana na international artistes ambao walipata shavu kama hilo kama David Guetta,Alicia Keys,Justin Bieber,Sean ‘Diddy’ Combs,Lebron James na Lady Gaga

SHULE YA MAPENZI NCHINI AUSTRIA


Kwa mara ya kwanza duniani nchini Austria kwenye jiji la Vienna, imefunguliwa shule ya kufundisha kufanya mapenzi aka World’s first international applied sex school
kiasi cha paundi 1,400 itatolewa kwa mwanafunzi atakayekaa hostel ambapo watakua wanafanya homework kabisa na Ylva-Maria Thompson, mkuu wa chuo hicho amefunguka kuwa elimu itakua inatolewa kivitendo zaidi

ELTON JOHN AMPASHAVU JUST TIMBERLAKE!!!

SIR ELTON HERCULES JOHN
Mkongwe wa Muziki toka Uingereza,Sir Elton John amefunguka kuwa ana mpango wa kumshirikisha Artist Justin Timberlake kwenye 'Biopic' yake aka movie inayohusu life story yake
JUSTIN RANDALL TIMBERLAKE
Kwa sasa kila kitu kiko kwenye mstari,na Director na crew nzima iko tayari wanasubiri script tu waanzae mambo na movie hiyo itakua na track zake mpya na Justin Timberlake,amekua chaguo lake la kwanza coz alisha act kwenye video ya Elton John ya David LaChapelle ‘Rocket Man’ na Elton john amechaguliwa kuwania tuzo kwenye Golden Globe zitakazofanyika January 15,2012 kupitia track yake ya Hello, Hello na ana mtoto wa kuasili yeye na 'husband wake' David Furnish aitwaye Zachary,aliyezaliwa December 25,2010

RAPPER JAY Z N LUDACRIS... BEEF KWAMBAAAL

CHRISTOPHER BRIAN BRIDGES - LUDACRIS
Imefunguliwa kuwa Baba Ivy Blue Carter aka Jay-Z wako kwenye ka-beef cha kiaina na Hip Hopper, Ludacris kuhusiana na kugombea eneo la biashara pande za Atlanta
SHAWN COREY CARTER - JAY Z
Jay-Z na Ludacris walikua wanawania sehemu pande Hartsfield-Jackson Airport-Atlanta,lakini airport hiyo ilikua na uwezo wa kumpangisha mtu mmoja na hatimaye Ludacris akalamba deal hiyo na kuamua kufungua Restaurant iitwayo Chicken N Beer

TOTO LA BEYONCE NA JAY Z

BABY BABA - JIGGA vs BABY MAMA - QUEEN B
Artist Beyonce Jigga Knowles na Rapper Jay Z,baada ya kuwa na uhusiano kwa miaka 6 na kufunga ndoa rasmi April 2008,wamepata motto wa kike waliyembatiza jina la Ivy Blue Carter jijini New York
Imefunguliwa kuwa Beyonce alijifungua pande za Lenox Hill Hospital,Ijumaa usiku baada ya kukodi ghorofa ya 4 sehemu ya hospitali hiyo kwa dola milioni 1.3 za kimarekani
Kabla ya kujifungua ma-doctor na ma-nurse wa hospitali hiyo walikatazwa kufika ghorofa ya 4 na wale waliokua pande hizo walinyanganywa simu zao ili wasiweze kupiga picha wakati Beyonce akijifungua

RIHANNA...BEST SELLING ARTIST

ROBYN RIHANNA FENTY - RIHANNA
R & B Star,Robyn Rihanna Fenty aka Rihanna amevalishwa taji la Queen wa kuuza mziki kwenye mtandao aka Best selling artist online
Ofisa toka kampuni ya Nielsen SoundScan amefunguka kuwa fans wali- download track za Rihanna mara milioni 47.5 kufikia mwisho wa mwaka 2012
BLACK EYED PEAS
Kundi la Black Eyed Peas limepata downloads milioni 42.4 kupitia track yao ya I Got Feeling huku Eminem wa 3 kwa kupata downloads milioni 42.2 na Lady Gaga ni wa 4 kwa kupata downloads milioni 42 na Taylor Swift downloads milioni 41.8
Pia artist Katy Perry,Lil Wayne,Beyonce,Kanye West na Britney Spears wamo kwenye Top 10

MSALA WA BEYONCE NA JAYZ

JAY Z vs BEYONCE
Celebz,Jay Z na Beyonce bila kujijua walisababisha shabiki wao mmoja kuchomwa kisu pande Ohio – Marekani baada ya kutokea mabishano juu yao
RONALD DEAVER
Issue ilianza baada ya jamaa mwenye miaka 48 kubishana na jamaa anayekwenda kwa jina la Ronald Deaver mwenye miaka 31,kwa kua alikua hana habari kama Beyonce ameolewa na Jay Z na mpaka kuwa na 'kitumbo' ndipo kulisababisha Ronald kumchoma kisu na kupelekea kukamatwa na maafisa polisi wa Ohio nchini Marekani

RAIS OBAMA ALIVYOJIACHIA HAWAII

RAIS BARACK OBAMA - MAREKANI
Rais wa Marekani,Barack Obama amebambwa na mtandao wa kimbea zaidi duniani akicheza american football,akiwa ametupia kapelo,pensi na akiwa tumbo wazi pande za Visiwa vya Hawaii
Rais Obama alikua kwenye mapumziko ya siku 10 ya mwisho wa mwaka yeye na familia yake kwenye kambi ya Kaneohe Marine Corps Base na alionekana akidaka mpira na kujiachia kwenye michanga kama kawa na alirejea hivi karibuni nchini Marekani baada ya holiday na kuanza mishe mishe za kampeni za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika November 6,2012

NDOA YA KOBE BRYAN


KOBE BEAN BRYANT
BasketBaller Kobe Bryant toka Los Angeles Lakers imefunguliwa kuwa ameichakachua ndoa yake kwa kutembea nje ya ndoa
KOBE & VANESSA BRYANT
Inadaiwa kuwa NBA star Kobe Bryant amemchakachua wife wake Vanessa Bryant aliyezaa nae watoto 2,kwa kutembea na wanawake wapatao 105 katika kipindi cha miaka 10 ya ndoa yao
....KOBE BRYANT FAMILY....
Vanessa alimkodi mtu kumpeleleza Kobe Bryant na inasemekana ameshakula uroda na rafiki wa Kim Kardashian,Carla DiBello,Playboy model Jessica Burciaga na actress Sanaa Lathan na kwa sasa Vanessa amewasilisha madai ya talaka na kwa mujibu wa sheria za California, mali zilizochumwa wakati wa ndoa hugawiwa nusu kwa nusu na utajiri wa Kobe Bryant unakadiriwa kufikia $ milioni 200

VI2KO VYA ARETHA FRANKLIN

BI ARETHA LOUISE FRANKLIN
Mkali wa muziki wa Soul toka Marekani,Aretha Loiuse Franklin mwenye umri wa maiak 69 amechumbiwa na long time friend wake William 'Willie' Wilkerson
....MAHARUSI WATARAJIWA....WILLIAM WILKERSON vs ARETHA FRANKLIN....
Aretha Franklin ambaye ni mshindi wa tuzo za Grammy alivalishwa pete na Wilkerson wakati wa mapumziko ya mwisho wa mwaka na kwa sasa mipango ya harusi inafanyika pande za Miami Beach,Florida na Bibi Aretha Franklin ana mpango wa kufanya sherehe ya watu wake wa karibu tu kwenye boti na anafikiria ma-designer kama Vera Wang,Valentino na Donna Karan wamtengenezee gauni lake la harusi na hii itakua ni ndoa yake ya 3 baada ya kuolewa mara 2 kabla

RICK ROSS AZINGUA NIGERIA

WILLIAM LEONARD ROBERTS II - RICK ROSS
Serikali ya Nigeria ina mpango wa kumshitaki Rapper toka Marekani,William Leonard Roberts II aka Rick Ross baada ya kushindwa kutia maguu na kupiga show kwenyetamasha maarufu la The Calabar Christmas Festival pande za Cross River State
Imefunguliwa kuwa Rick Ross alishakula mkwanja wake na haijajulikana sababu ya kutokwenda kupiga show serikali ya Cross River State kwa sasa imekodi mwanasheria toka Marekani kwa ajili ya kumfungulia mashitaka Rick Ross

NICK CANNON

NICK CANNON....KWA HOSPITAL
Baada ya kulazwa ghafla hospitali kwa matatizo ya figo,Nick Cannon amefunguka kupitia mtandao wa twitter kuwa ameshafanyiwa upasuaji
Kwa sasa Singer,actor na TV star,Nick Cannon anaendelea poa na amewashukuru fans wake kwa kumuombea

BIFF ZA MTONI

RAPPER DMX....AVAMIWA KWENYE STAGE...!

EARL SIMMONS - RAPPER DMX
Rapper DMX,amepata msala alipokua anapiga show pande za Cafe Sevilla,Long Beach-California baada ya fan wake mmoja kuruka kwenye stage na kumvaa Wakati DMX anaanza kuimba track yake ya One More Road to Cross iliyokua kwenye album yake ya 3 aliwauliza fans wake "Are you ready to get this shi* started for real?....ndipo jamaa alivamia stage na na kumkaba shingoni kabla ya security kumuokoa DMX na mumtoa kwenye stage
0 comments

REDSAN:: MALAIKA REMIX

ARTIST REDSAN.....KUPIGA REMIX YA MALAIKA...!

SWABRI MOHAMED - REDSAN
Baada ya Artist kibao duniani kama Brothers Four,Helmut Lotti,Miriam Makeba,Harry Belafonte,Boney M,Usha Uthup,Angélique Kidjo kutengeneza version zao za wimbo maarufu toka Kenya,Msanii Redsan kwa sasa ameungana nao kiaina coz inafunguliwa kuwa naye yuko kwenye mishe za kugonga remix ya Malaika aka famous African ballad
FADHILI WILLIAM MDAWIDA
Redsan kwa sasa yuko studio akigonga remix ambayo wadau wanafunguka kuwa itamrudisha kwa kishindo kwenye tasnia ya muziki Afrika Mashariki na ngoma hiyo ya Malaika ilifanywa na Msanii Fadhili William toka Kenya akiwa na Bendi yake iliyoitwa Jambo Boys kwenye miaka ya 60
1 comments

TATOO INDA CHURCH

ASTOR AFUNGUA SEHEMU YA TATOO...KANISANI..!

....MUUMINI AKICHORA TATOO....
Katika kubuni njia ya kuwavutia waumini waje kwa wingi kanisani kwake,Pastor mmoja ameamua kufungua sehemu ya kuchora tatoo na kufundisha kupigana kanisani
....KITU CHA TATOO CHA PASTOR....
Pastor Steve Bentley wa kanisa la The Bridge Misteries toka Michigan- Marekani maeamua kufungua tatoo parlour kama sehemu ya kuhamasisha waumini wake waje kanisani kwa wingi na kwa sasa amewaajiri wafanyakazi wawili,Ryan Brown na Drew Blaisdell ambao wanafanya kazi kwa appointment maalum kuanzia mchana mpaka saa 2 usiku,Jumatatu mpaka Jumamosi na katika kuonesha msisitizo yeye mwenyewe pastor ameshatupia tatoo 2 za nguvu

JAY Z WIC BLUE IVY

JAY - Z....ATOA NGOMA KWA MTOTO WAKE...IVY!

SHAWN COREY CARTER - PAPA IVY BLUE
Baada ya kupata mtoto Ivy Blue Carter over the weekend yeye na wife wake Beyonce,Papa Hov ameachia ngoma kwa ajili ya mtoto wake huyo iitwayo Glory ft B.I.C kupitia website yake ya Life + Times
Kwenye ngoma ya Glory,Jigga ameonesha hisia zake juu ya mtoto wake huku mwisho ameweka sauti ya mtoto wake Ivy Blue Carter na pia amefafanua kwa nini wamemuita mtoto wao blue coz blue ni rangi anayoipenda zaidi pia kwa kutoa alnum ya The Blueprint 2 mwaka 2002 na The Blueprint 3 mwaka 2009 kuonesha kuizimia zaidi rangi ya blue

OMBEA WAKONGWE WA FANI

...IT'S ALL ABOUT HIP HOP...!

...IT'S ALL ABOUT HIP HOP...!

GOD BLESS THE DEAD..........!

GOD BLESS THE DEAD..........!

FAZA NELLY

FAZA NELLY

GERALD SABAI aka MR THRILL (1973 - 2011)

GERALD SABAI aka MR THRILL (1973 - 2011)

PIMP C

PIMP C

MAC DRE

MAC DRE

BIG PROOF

BIG PROOF

BIG L

BIG L

OL DIRTY BASTARD

OL DIRTY BASTARD

JAM MASTER JAY

JAM MASTER JAY

EAZY E

EAZY E

NOTORIOUS BIG

NOTORIOUS BIG

2 PAC SHAKUR

2 PAC SHAKUR

REMEMBER "KING OF POP"

REMEMBER "KING OF POP"

REMEMBER "BOB MARLEY"

REMEMBER "BOB MARLEY"

....NATE DOGG...!

....NATE DOGG...!

NEW TRACK: STAR JAY FT COYO MC - MACOPA

NEW TRACK: MacMillz Ft GQ - Bata Day ( RACERS STUDIOS)

HI NDO TRACK YAKE MPYA YA 2012